November 28, 2012


Waasi wa M23 waanza kuondoka Goma

Mkuu wa vikosi vya usalama vya Umoja wa Mataifa, Herve Ladsous, amesema kuwa kuna dalili waasi wa M23 wanaanza kuondoka mji wa Goma.

Lakini aliongeza kuwa hali ingali ya wasiwasi na kuwa inaweza tu kuthibitishwa na majeshi ya Umoja wa Mataifa yanayoshika doria.
Kiongozi wa waasi hao, Sultani Makenga, alisema kuwa waasi wataondoka Goma siku ya Ijumaa.
Lakini kuna ripoti kuwa huenda tawi la kisiasa la kundi hilo likasalia mjini humo.