Wasi wasi kuhusu virusi vya ugonjwa hatari wa Ebola
Utafiti wa wanasayansi kutoka Canada unaashiria kuwa aina hatari zaidi ya virusi vya Ebola inaweza kusambazwa hewani kati ya aina mbili ya viumbe.
Matokeo ya utafiti huo, yanasema kuwa nguruwe waliokuwa wameambukizwa aina ya Ebola kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, waliweza kuiambukiza kwa nyani, bila ya kugusana.
Watafiti hao wanadhani maambukizi ya aina hiyo yanachangia kusambaa kwa ugonjwa huo hatari barani Afrika, na kwamba nguruwe huenda wanabeba virusi hivyo.
Lakini wanaamini ugonjwa huo unaweza tu kusambazwa katika eneo dogo, na hauwezi kusambaa haraka kama homa.
Nchini Uganda, mlipuko mpya wa Ebola umewauawa watu wawili karibu na mji mkuu, Kampala.
Virusi vya ugonjwa huop wa Ebola, husababisha vifo kwa bvinadamu na viumbe vingine mbali na binadamu.
Matokeo ya uchunguzi huo yamechapishwa kwenye jarida ya kimatibabu nchini humo ili kuelimisha jamii husika.
Kwa mujibu wa Shirika la afya duniani WHO, maambukizi miongoni mwa binadamu husambazwa kwa watu kukaribiana, kupitia damu, unyevu mwilini na maji maji yanayotokana na wanyama wengine kama vile, sokwe na Swara.
Popo pia aweza kuwa chanzo cha maambukizi hayo ya viruso vya ebola.
Lakini baada ya utafiti kufanywa, imebainika kuwa nguruwe wanaofugwa nyumbani au wale wa mwituni wanaweza kuwa vyanzo vya virusi hivyo ambavyo ni hatari zaidi kwa uhai wa binadamu.