December 18, 2012



CHUONI WAPIGA WAAMUZI, KOCHA WAO


Na Abdi Suleiman, Pemba 
SAKATA la waamuzi wanaochezesha ligi daraja la pili Taifa Pemba kupigwa na wachezaji, limeendelea kurindima baada ya juzi mwamuzi mwengine kujikuta akiangushiwa kisago na wachezaji wa timu ya Chuoni.

Kasheshe hiyo imetokea katika uwanja wa Msaani, baada ya timu ya chuoni kufungwa magoli 2-1 na timu ya Nuru Boys, na kuamua kuhamishia hasira zao kwa mwamuzi wa pambano hilo, Ali Said na msaidizi wake nambari mbili Amour Ali.

Na katika hali isiyotarajiwa, wachezaji hao pia walimpa kichapo kocha wao Yahya Ali, aliyekuwa akiamua vurugu hizo zilizosababishwa na wachezaji wake. Wachezaji hao waliamua kuwachapa waamuzi baada ya kupuliza firimbi ya kumaliza mchezo, kwa madai kuwa, alivunja mechi hiyo kabla ya wakati wake.

Akizungmza na mwandishi wa habari hizi, baada ya kumalizika kwa tafrani hiyo, mwamuzi huyo alisema kuwa, katika vurugu hizo pia saa yake ya mkononi ilichukuliwa na wachezaji wa timu hiyo kutokana na vurugu walizofanya. 
Mwamuzi huyo aliwataja wachezaji saba waliohusishwa na kadhia hiyo kuwa ni, Mohammed Bakari, Suleiman Ashrib, Ali Abdulrahman, Khamis Nassor, Said Ashrib, Seif Hamad na Nassor Mohamed.

Akizungumzia sakata hilo, Msaidizi Katibu wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) Taifa (Pemba)  Abdallah Suleiman Sharif, amekiri kusikia taarifa hiyo, na kusema kuwa taarifa kamili itatolewa baada ya kamati tendaji kupitia ripoti za  mwamuzi na kamisaa.


Hata hivyo, ameelekeza lawama kwa Jeshi la Polisi, kutokana na kutopeleka askari uwanjani kwa ajli ya kuweka ulinzi, licha ya chama chake 

SAY IT WITHOUT SAYING IT.!


Meneja wa Kampuni ya Kioo Ltd Bw. Kishir, akipokea oda ya vinywaji vikali vya Johnnie Walker kutoka kwa balozi wa vinywaji vikali wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd   baada ya kufanya oda hiyo na kufungiwa kwenye mfumo mzuri wa zawadi. Hafla hiyo imefanyika mapema leo katika ofisi za Kioo Ltd zilizopo Chang’ombe,jijini dar.  Kampeni hii ya kutoa zawadi za mwisho wa mwaka zinaendeshwa kwa msemo usemao ‘Say it Without Saying it’. Maana yake toa zawadi kwa uwapendao badala ya kusema kwa maneno. Hivyo za wadi ya Johnnie Walker ndio muafaka kwa kipindihiki

MSANII WA FILAMU SAJUKI AANGUKA JUKWAANI ARUSHA

HALI ya msanii wa filamu nchini,Juma Said Kilowoko maarufu kama Sajuki imeelezwa si ya kuridhisha mara baada ya msanii huyo juzi kuanguka jukwaani kwa  kuishiwa nguvu wakati alipopanda jukwaani  kuwasalimia mashabiki waliofurika kumtizama. 

 Tukio hilo lilitokea Jumapili katika tamasha la wasanii wa filamu na wale wa muziki wa kizazi kipya lililofanyika ndani ya uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid wakati msanii huyo alipopandishwa jukwaani kuwasalimia mashabiki wake.

 Mara baada ya msanii huyo kupandishwa jukwaani alipewa kipaza sauti ili aweze kuwasalimia mashabiki wake lakini katika hali ya kawaida alifanikiwa kutamka neno moja tu”ahhh" na kisha kudondoka chini ya jukwaa lakini kabla ya kutua chini alidakwa na wasanii waliokuwa pembeni yake. 

Wasanii wenzie walimkalisha chini ya jukwaa hilo ili aweze kupumzika na kisha baada ya muda mfupi walimshusha chini ya jukwaaa hilo ili aweze kupata muda wa kupumzika zaidi. 

 Akihojiwa  muda mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki kwa sauti ya upole alisema kwamba hali yake kiafya si nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji matibabu zaidi. ”Kaka hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana sijisikii vizuri”alisema Sajuki huku akionekana mnyonge zaidi
Sajuki akipumzika kwa muda baada ya kuanguka
Sajuki akinyanyuliwa
Akitelemshwa toka jukwaani

TAARIFA ZA HALI YA HEWA SASA KUPATIKANA KWA NJIA YA SIMU

Mkuu wa Kitengo cha Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani namna huduma ya upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa kuanzia sasa itakavyofanyika kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini na Kampuni ya Vodacom, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dk Agnes Kijazi.
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA