December 14, 2012

Godfrey Chitalu, mchezaji wa Zambia mwenye rekodi kubwa ya mabao kwa mwaka
Godfrey Chitalu pia alikuwa kocha wa timu ya Taifa ya Zambia
Shirikisho la soka la Zambia, linasema linataka shirikisho la soka duniani FIFA kutambua mcheza soka wa nchi hiyo Godfrey Chitalu kwa uhodari wake wa kupachika mabao 107 kwa mwaka mnamo mwaka 1972.
Hatua hii inakuja baada ya gwiji wa soka anayeshikilia rekodi ya Dunia kwa uchezaji bora, Muajentina Lionel Messi kuvunja rekodi ya mcheza soka mjerumani Gerd Mueller aliyefunga mabao 85 katika mwaka mmoja.
 Messi hadi sasa ameshafunga mabao 88 mwaka huu pekee.
Msemaji wa shirikisho la soka la Zambia, Faz, Eric Mwanza, aliambia BBC kuwa wana rekodi za kuthibitisha kuwa Chitalu anapaswa kutambuliwa kwa mabao aliyofunga mwaka huo kwani hadi sasa hakuna aliyekwisha vunja rekodi hiyo !.
"tunamtumia ujumbe, katibu mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, kuangalia upya swala hili la Godfrey Chitalu." Bwana Mwanza alisisitiza.
Baada ya maisha yake kama mchezaji wa soka, Chitalu alichukua wadhifa wa kocha na hivyo kuanzisha timu ya Taifa ya Zambia.
Timu ya taifa ya soka Zambia
Alifariki pamoja na wachezaji wengine 29, 18 miongoni mwao wakiwa wachezaji wa kimataifa, katika ajali ya ndege katika pwani ya Gabon walipokuwa wanakwenda Senegal kwa mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia Mwaka 1993.
Bwana Mwanza pia aliongeza kuwa mwaka 1972, haikuwa ndio mara ya kwanza kwa Chitalu kucheza vizuri kabisa.
"katika msimu wa ligi kabla ya mwaka 1972, aliingiza mabao 89 ," bwana Mwanza alielezea zaidi.
Mnamo mwaka 1972, alifunga mabao 107, yaliyohusisha mechi za ligi , mechi za vilabu , mechi za kitaifa pamoja na mechi za kirafiki''
Rais wa Faz, Kalusha Bwalya, alisema kuwa anakumbuka vyema sana alivyocheza bwana Chitalu.
''Kwa hivyo ingekuwa muhimu sana kumtambua kwa umahiri wake wa kufunga mabao,'' alisema Bwalya ambaye kwa sasa ndiye kocha Mkuu wa kikosi chaTimu ya Taifa ya Zambia.
Baadhi ya wachezaji wa zamani maarufu kwa soka ni pamoja na Pele, Platini, Maradona ,Van Basten na wengine wengi.............