Kuishi miongoni mwa waasi huko DRC...!
Waasi wa M23 walioko Mashariki mwa DRC, wamegonga vyombo vya habari sana katika miezi michache iliyopita, wao ni moja tu na makundi mengi ya waasi wanaopigana katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa.
Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la misaada la OXFAM, limeonyesha kuwa hiki ni kionjoo tu cha masaibu yanayowakumba wananchi wa kawaida
Harakati zao zilianza mwezi Mei wakati walipoasi jeshi la taifa. Kulingana na umoja wa matifa, walipokea msaada mkubwa kutoka kwa Rwanda , madai ambayo serikali ya rais Kagame imekanusha vikali.Waasi hao ambao jina lao lilitokana na juhudi za amani za terehe 23 mwezi Machi na ambazo hazikufua dafu, waliuteka mji wa Goma wiki mbili ziliopita kabla ya kuondoka mjini humo mwishoni mwa wiki na mali walizopora . Sasa wako nje ya mji huo.
Tisho la waasi wa M23 kwa mji wa Goma , bila shaka lilisababisha mabadiliko, wasiwasi jeshini na kusababisha hatua za haraka kwani vikosi vya UN pamoja na jeshi la DRC walishirikiana kupambana nao.
Hatua hii nayo ilisababisha pengo la kiusalama katika maeneo mengine ambayo yana makundi madogo maodgo ya waasi.
Kodi kwa waasi
Zaidi ya makundi 25 ya waasi, yanaendesha harakati zao katika mikoa miwili Mashariki mwa DRC. Kivu Kaskazini na Kusini. Wanadhibiti maeneo mengi lakini hasa yale yenye rasilimali nyingi na ambako wasafiri wanweza kutozwa kodi.
Soko dogo la Kashanga lililoko kaskazini mashariki mwa Goma... lilishambuliwa mara kumi na mbili kati ya mwezi ya Aprili na Julai mwaka huu.
Waasi wanavamia watu na kuwapora mali zao, kulingana na OXFAM
Katika miaka ya hivi karibuni, makundi ya waasi katika eneo la kivu yameongezeka sana . Sio nadra kukutana na makundi matatu yakipigania barabara moja.
Makundi haya kuwaruhusu waandishi kupita kwa hofu ya kuvutia shauku.
Lakini raia hawana bahati , wao huvamiwa na wakati mwingine kuuawa.
Makabiliano kati ya makundi hayo pia sio nadra. Hupigania kodi wanazowatoza wananchi ambao ni wafanyabiasha wadogo katika masoko. Na yeyote anayepinga makundi hayo au hata kupinga mayowe kutafuta usaidizi, huuawa.
Katika maeneo ya Kivu takriban watu zaidi ya laki saba wameachwa bila makao.
Mashirika ya kibinadamu yanasema kuwa huu ni mzozo mkubwa wa kibindamu ambao dunia haiwezi kuendelea kupuuza.
Matajiri kiasi cha kutojali
Lakini licha ya mashirika ya kibinadamu yanavyosema, ukweli ni kuwa watu wengi kote duniani , wanapuuza matatizo ya DRC.
Habari zinazotoka nchini humo daima ni za kuhuzunisha kiasi cha watu kuzoea kuzisikia wala hawaoni maana au ikiwa ni muhimu kuchukua hatua.
DRC ni nchi ya kupendeza mno.
Ina milima chungu nzima, mchanga wenye dhoruba na ambao unaweza kuzalisha chakula kwa mifugo ,kuna madini ikiwemo, dhababu na coltan ambayo hutumiwa kutengeza vifaa vya elektroniki, hali ambayo imechangia idadi kubwa ya watu.
- Idadi kubwa ya watu wa makabila ya Tutsi na Hutu waliohamia maeneo hayo, ya Kivu, kumeathiri idadi ya watu wa makabila mengine wanaoishi hapo.
- Nchi jirani zinatumia udhaifu wa taasisi za DRC kupora mali ya nchi hiyo.
- Maeneo ya Kivu yako umbali wa kilomita 1,500 kutoka mji mkuu wa Kinshasa. Hali hii huchochea muingilio wa nchi za kigeni kwa hali ya DRC
Watu wengi wametoroka makwao, mara nyingi wakati wa miaka mingi ya migogoro katika eneo hilo kulingana na shirika la OXFAM.
Hali ni mbaya kwani mamia ya watu wanakwenda vitandani kila usiku kwa hofu ya kushambuliwa, kuporwa , kuuwawa au kutekwa nyara, huku wanawake wakihofia kubakwa.
Mashirika ya kibindamu yametoa wito kwa serikali ya DRC pamoja na UN kujibu tuhuma za raia wa kawaida kuathiriwa zaidi na hali ya vita DRC
Lakini cha muhimu zaidi ni kwamba ukarabati utahitajika kwani hakuna hata moja ya taasisi hizi imeweza kukidhi mahitaji ya raia.
Mfano wakati Sierra Leone ilikabiliwa na changamoto kama hizi, ililazimika kujijenga upya kuanzia kwa jeshi na kisha taasisi zingine.
Lakini tatizo la DRC ni kwamba ina utajiri mkubwa sana hali ambayo ni changamoto kubwa kwa ukarabati wa nchi.
Huenda washirika wengi wa DRC wanafaidi sana kutokana na mali ya nchi hiyo na hivyo hawana nia ya kurejesha utulivu kupitia kwa jeshi
Wanafaidi sana kutokana na vita vya sasa.