December 09, 2012

HATIMAYE TRENI YA KWANZA DAR - MWANZA YAWASILI MWANZA SALAMA MARA BAADA YA KUSITISHWA SAFARI ZAKE MIAKA 3 ILIYOPITA.

WANANCHI WAMSIFU WAZIRI MWAKYEMBE.. 

Wakati leo Tanzania inasherehekea miaka 51 ya Uhuru wake, jiji la Mwanza linashuhudia safari ya treni ya kwanza ya abiria ikiwasili jijini hapa kutokea kituo cha kwanza jijini Dar es salaam,  tangu mara ya mwisho ilipositishwa takribani miaka mitatu iliyopita kutokana na wawekezaji waliopewa dhamana kipindi hicho kushindwa kuliendesha shirika la utoaji huduma hiyo.