Jeshi la Sudan Kusini lauwa Raia 10
Umoja wa Mataifa umesema kuwa jeshi la Sudan Kusini limewapiga risasi na kuwauwa watu 10,ambao walikuwa wakiandamana kupinga kuhamishwa kwa makao makuu ya serikali za mitaa magharibi mwa nchi hiyo.
Afisa wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Bahr el-Ghazal amesema watu wanne waliuawa katika mji wa Wau kwenye mapambano ya jana usiku na wengine sita waliuawa baada ya kukusanyika kulalamikia juu ya mauaji ya wenzao waliouawa awali.
Jeshi la Sudan Kusini limekataa kusema kitu chochote juu ya mauaji hayo.