December 19, 2012


MHE PINDA ZIARANI JIMBONI KATAVI

 Waziri mkuu Mhe Mizengo Pinda akizindua mradi wa  madawati kwa kukata utepe katika kijiji cha Inyoga mkoani Katavi. Kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa Katavi Dr Rajabu  Rutengwe na kushoto ni mwenye kiti wa kijiji cha Inyogo bwana Athony Kanyika. Mhe Pinda, ambaye ni mbunge wa jimbo la katavi,  yupo  jimboni kwa ziara ya kukagua  shughuli za maendeleo.
Waziri mkuu Mhe Mizengo Pinda amepewa heshima ya kimila kwa kuvishwa kofia na kukabidhiwa mkuki na wazee wa Inyonga kama ishara ya kutambua mchango wake aliowaletea wananchi wa mkoa wa Katavi. Picha na Chris Mfinanga