UPDATE YA KESI YA LEMA:
WAKILI wa Serikali Mkuu Timon:
Korti ilikosea kumvua Lema ubunge
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (wapili kulia) akiambatana na wafuasi wa Chadema wakitoka nje ya Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam jana, baada ya kusikilizwa rufaa yake ya kupinga kuvuliwa ubunge wake. Picha na Michael Jamson
Wakili Vitalis alitoa madai hayo jana, wakati wa usikilizwaji wa rufaa ya Lema, aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),katika Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam.
Wakati wakili huyo wa serikali akitoa madai hayo, Wakili wa wajibu rufaa, ambao walishinda katika kesi ya msingi, Alute Mughway, naye alidai kuwa Mahakama Kuu, Arusha ilikosea katika uamuzi wake, pamoja na mambo mengine, kwa kukataa baadhi ya madai yao.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea........>>>>>>