WAZIRI WA ARDHI PROF. ANNA TIBAIJUKA AINGILIA KATI MGOGORO KATI YA WAKAZI WA KATA YA BUNJU NA KIWANDA CHA SARUJI CHA TWIGA - WAZO
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka akiongea katika mkutano wa hadhara na maelfu ya wakazi wa kata ya Wazo na Bunju waliojitokeza kufuatilia maendeleo ya mgogoro wa ardhi kati yao na Kiwanda cha Twiga Cement ambapo pamoja na mambo mengine amewahakikishia wakazi hao kuwa mgogoro huo utapatiwa ufumbuzi wa kudumu na kuwaomba kutoa ushirikiano kwake.
Sehemu ya umati mkubwa wa wakazi wa kata za Bunju na Wazo wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka (kulia) akiongea na Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Saruji cha Twiga (Twiga Cement) Bw.Pascal Lessoinne (kushoto) mara baada ya mkurugenzi huyo kutoa taarifa fupi ya maendeleo ya kiwanda hicho na hali ya mvutano wa muda mrefu wa umiliki wa maeneo baina ya wakazi wa kata za Bunju na Wazo jijini Dar es salaam.