December 05, 2012


WAZIRI WA UCHUKUZI Dkt. HARRISON MWAKYEMBE ADAKA WATUMISHI WATANO WA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA (TPA) WAKITAKA KUVUSHA MALORI 26 KINYEMELA BANDARINI !



Waziri wa Uchukuzi Dk. Harisson Mwakyembe akizungumza na waadishi wa habari Bandarini jijini Dar es salaam Jana  jioni wakati akitoa taarifa ya kukamatwa kwa watumishi wa Bandari wanaodaiwa kutaka kutoa  malori 26 kinyemela  bandarini, watu watano wamekamatwa katika sakata hilo.
Afisa Utawala wa kampuni ya Dhandho Antipasi Otieno (kulia) akitoa maelezo mbele ya waziri Dk. Harrison Mwakyembe

Dk. Mwakyembe akikagua Malori yanayodaiwa kutaka kutolewa kinyemela na kampuni ya Dhandho, Malori matano kati ya 26 yalipewa baraka na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yatolewe.