Ushahidi mpya wa mauaji ya Mau Mau
Baadhi ya wapiganaji wa Mau Mau waliodhulumiwa na wakoloni wa Uingereza
Stakabadhi za Serikali zilizotolewa huko Uingereza zinaonyesha kwa ukamilifu namna wafungwa wengi waliuawa wakati wa uasi wa kundi la Mau Mau nchini Kenya.
Wakenya kumi na mmoja walipigwa na walinzi hadi kufa katika kambi walikozuiliwa ya Hola huku wengine wakijeruhiwa mnamo mwaka 1959 wakati wa vita ya Mau Mau thidi ya Mkoloni.
Mzee mmoja aliyenusurika kifo katika mauaji hayo kwa sasa ameshtaki serikali ya Uingereza akidai kwa kuteswa na kuhatarishiwa maisha.
Stakabadhi hizo zinaonyesha mkutano uliongozwa na aliyekuwa gavana wa Kenya na maafisa wakuu wa magereza wakati huo.
Kumbukumbu zinazoonyesha kuwa maafisa hao walikiuka haki za binadamu lakini hawakufunguliwa mashtaka hadi leo !.
bbc