January 21, 2013


UKUTA WAANGUKIA MAGARI NA KUyaharibu VIBAYA, ni NDANI YA KITUO CHA MABASI chA UBUNGO BUS TERMINAL ni mapema leo JIJINI DAR.

zaidi ya gari 40 zimeharibika vibaya sana shuhudia mwenyewe.

Ukuta wa eneo la ndani ya kituo cha Mabasi ya Ubungo Bus Terminal  umeangukia magari zaid ya 19 (baadhi kama uonavyo pichani) zikiwemo bajaji  tatu,yaliyokuwa yamepaki eneo  ambalo hutumika kupaki  wakiwa wanasindikiza abiria na ndugu zao,aidha chanzo cha ajali hiyo kimeeleza kuwa ni Mkandarasi wa eneo hilo aliyekuwa  akibomoa ukuta huo,na pia imeripotiwa kuwa kuna baadhi ya majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali kwa matibabu.

Baadhi ya Maofisa kutoka Jeshi la Polisi wakiangalia baadhi ya magari yaliyoathiriwa vibaya mara baada ya kuangukiwa na ukuta mapema leo asubuhi kwenye eneo la kupaki magari,ndani ya kituo kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani.Ukuta huo ulikuwa ukibomolewa na Mkandarasi ikiwa ni hatua za awali wa kituo hicho kuvunjwa kwa ajili ya kupisha mradi wa ujenzi wa mabasi yaendayo kasi.
Pichani juu ni baadhi ya magari mbalimbali yalioyoathiriwa vibaya kufuatia kungukiwa na ukuta.
Si Magari tu,hata bajaji pia zimeathiriwa vibaya kama uonavyo pichani.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, KinondoniAfande Charles Kenyela akitoa maelekezo mafupi kwa baadhi ya maofisa wa Polisi waliokuwa wamefika kwenye eneo la tukio mapema leo asubuhi.