January 21, 2013

COSMOS GROUP WAZINDUA JENGO JIPYA LA UHURU HEIGHTS JIJINI DAR LEO

Mgeni rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa jengo la Uhuru Heights,Balozi wa Pakistan nchini Tanzania,Tajammul Altaf akizungumza katika uzinduzi huo ambapo amasema amefurahishwa na jitihada zilizofanywa na mfanyabiashara kutoka nchini kwake na jinsi Tanzania ilivyoweza kumpa ushirikiano na hatimaye sasa matunda yameonekana kwa kuzaliwa jengo la Uhuru Heights lenye hadi ya Kimataifa.Aidha amesema huo ni mwanzo tu na kuwataka wafanyabiashara zaidi kutoka Pakistan kuja kuwekeza Tanzania kwa sababu mahali ambapo ukiwekeza matunda yanaonekana kutokana na amani na utulivu uliopo na ushirikiano wa serikali.
Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights, Muhammad Owasi Pardesi akizungumza na wageni wakati wa uzinduzi wa jengo hilo na kutoa shukrani zake akisema sasa wakazi wa Dar es Salaam wataweza kununua nyumba kwa njia ya mkopo kutoka Benki ya International Commercial (ICB) na kulipa kwa muda wa miaka 10 na kuishi katika miongoni mwa majengo marefu ya makazi yaliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam lililojengwa kwa gharama ya Dola za Kimarekani Bilioni 40.
Amesema Malengo ya kampuni ya Cosmos Group ni kuboresha miundo mbinu na maisha ya watu na hayo yamezingatiwa kwa kujenga jengo la Uhuru Heights.
Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights Muhammad Owasi Pardesi akipeana mikono na Afisa Mtendaji Mkuu wa International Commercial Bank (Tanzania) LTD Basser Mohamed (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya EXIM Anthony Grant (kushoto) ikiwa ni ishara ya kuingia mkataba wa kufanya biashara pamoja baina ya Cosmos, IBC Benki na Exim.
MC 
Taji Liundi 
katika uzinduzi wa Jengo la Uhuru Hegihts .

MUONEKANO WA JENGO LA UHURU HEIGHTS LILILOPO BARABARA YA BIBI TITI MOHAMMED LIKING'ARISHA JIJI LA DAR NYAKATI ZA USIKU.

ATCL KUANZA SAFARI ZAKE ZA ANGA RASMI KESHO

Wahandisi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakikamilisha kufunga kioo kipya ambacho kimenunuliwa kutoka nchini Marekani cha ndege yao aina ya Dash-8 Q300 yenye namba za usajili SH-MWF ambayo ilipata ufa (Wind shield crack) tarehe 11 Januari, 2013, muda mfupi baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Kigoma kurudi Dar Es Salaam katika safari zake za kawaida. 
Matengenezo hayo yanafanyika katika uwanja wa ndege wa Kigoma yakisimamiwa na Mhandisi Righton Mwakipesile na Mhandisi Merkior Karwani.
Uongozi wa ATCL umedhibitisha kuwa safari za Dar-Kigoma-Dar zitaendelea kama ratiba yao inavyoonyesha punde kuanzia kesho tarehe 22/1/2013. 

HATIMAE BI ARAFA AFANYIWA UPASUAJI NA ANAENDELEA VEMA KATIKA HOSPITAL YA MUHIMBILI

Kwa Niaba ya Familia ya Bi Arafa (Pichani) Napenda kutoa shukrani za Dhati kwa wale wote ambao waliguswa na hali ya Mgonjwa huyu na kuridhia kumchangia ili kumtoa wilayani Ruangwa na kuwezesha kumfikisha katika Hospital ya Muhimbili Mwezi Nov 2012 na juzi kufanyiwa Upasuaji.

Hali ya Mgonjwa huyu inaendelea vema katika hospital ya Muhimbili akisubiria kutoa Nyuzi

Mungu aliwawezesha na kumsaidia mpaka hali ilivyofikia sasa na Kubwa Nawaomba Muendelee kumuombea Dua ili aweze kupona na kuendelea kujitafutia riziki ya kila siku

Ahsanteni sana.
Ni Mimi Abdulaziz Ahmeid Video

MH. SAMUEL SITTA, OFISI YA MWANASHERIA MKUU, TUME YA KUREKEBISHA SHERIA NA WAZEE KWA PAMOJA WATOA MAONI KATIBA MPYA LEO

Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Waziri wa Afrika Mashariki Mhe. Samwel Sitta akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano baina yao katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (jumatatu januari 21, 2013). Kushoto ni Mjumbe wa Tume Bi. Maria Kashonda.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Afrika Mashariki Mhe. Samwel Sitta (katikati) akiagana na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi (kushoto) na Bw. Nassoro Mohammed (kulia) mara baada kiongozi huyo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Mashtaka Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika mkutano kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (jumatatu januari 21, 2013) jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju na Wajumbe wa Tume Bw. Humphery Polepole na Bw. Awadhi Said.
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Mohammed Hamad akitoa ufafanuzi kuhusu majukumu ya kitengo cha utafiti cha Tume kwa ujumbe wa Tume ya Kurekebisha Sheria (LRCT) ulioongozwa na Makamishina wa Tume hiyo, Jaji Ernest Mwipopo (wa tatu kulia) na Bi. Esther Manyesha (wa nne kulia). LRCT imewasilisha maoni kuhusu Katiba Mpya kwa Tume leo
Kamishina wa Tume ya Kurekebisha Sheria (LRCT) Jaji Ernest Mwipopo akikabidhi maoni ya LRCT hiyo kuhusu Katiba Mpya kwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Prof. Mwesiga Baregu katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (jumatatu januari 21, 2013). Katikani ni Mjumbe wa Tume Bw. Simai Mohammed.
Mjumbe wa Mtandao wa Kinga Jamii (TPSN - Tanzania Social Protection Network) Bi. Clotilda Isdor akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko uliofanyika leo (jumatatu janauari, 21, 2013). Wa kwanza kushoto ni Mjumbe wa Tume, Bi. Mwatumu Malale.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi aliloandaliwa kwa heshima yake mjini Paris Ufaransa leo Januari 21, 2013 ikiashiria kuanza rasmi kwa ziara yake ya kiserikali ya siku tano nchini humo
 Gari iliyomchukua Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikiondoka Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi aliloandaliwa kwa heshima yake mjini Paris Ufaransa leo Januari 21, 2013 ikiashiria kuanza rasmi kwa ziara yake ya kiserikali ya siku tano nchini humo
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akiwa katika maongezi rasmi na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa na ujumbe wake  katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa baada ya mazungumzo yao rasmi katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa wakiongea na wanahabari baada ya mazungumzo yao rasmi katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013.
PICHA NA IKULU

Makatibu wa Bunge wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika mwishoni mwa wiki wamekutana Kampala,Uganda kupitia Kanuni za vikao vyao pamoja na Mpango Mkakati wa Kundi lao ambalo ni moja ya vitengo vya Chama cha Wabunge wa Jmuiya ya Madola Kanda ya Afrika. Katika Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na Makatibu wa Mabunge ya Ghana, Botswana,Uganda,Nigeria, Kenya,Afrika Kusini na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Sekretarieti ya Chama hicho iliwakilishwa na Nd. Saidi Yakubu (kwanza kushoto waliosimama) na Nd. Demetrius Mgalami (wa tatu kushoto waliokaa) na Nd. Hassan Amour wa Baraza la Wawakilishi (wa tatu kushoto waliosimama). PICHA KWA HISANI YA SEKRETARIETI YA CPA KANDA YA AFRIKA.JK AENDELEA NA ZIARA YAKE NCHINI UFARANSA.
                LEO KUKUTANA NA MWENYEJI WAKE, RAIS WA UFARANSA


 Mwenyekiti wa Jumuiya wa Watanzania waishio Ufaransa Deli Makombe akisoma risala meza kuu
 Rais Kikwete akiongea na wananchi waishio Ufaransa
 Balozi Dorah Msechu kushoto katika pozi na mdau
kicheko kidogo
 Mama Salma Kikwete akisalimia kadamnasi
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akihutubia
 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk akiongea
 Waziri na Nishati na Madini Profesa Sospeter  Muhongo akiongea
 Baadhi ya wadau waking'amua matukio kimyakimya... 
 Waziri wa Ujenzi Dkt John Pome Magufuli akiongea na hadhara 

 JK akifurahi na watoto
 JK na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Ufaransa
 JK na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na maafisa wa ubalozi

 Dkt Magufuli akifurahia jambo ktk mazungumzo 
 Prof Muhongo akiongea na wadau
 JK akiongea na wadau
 Profesa Mohamed Sheya, Naibu Mwakilishi wa kudumu Unesco katika jumuiko hilo.
 Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa akisema machache
Baadhi ya maafisa kutoka Tanzania walioongozana na Rais Kikwete katika ziara hiyo nchini Ufaransa.