April 29, 2013

SEHEMU YA PICHA ZA ZIARA YANGU KANDA YA ZIWA

Usafiri kama kawaida ukawa wa siku zote HEWANI NA FAST JET.

Hewani majumba yanaonekana kama picha hizi juu na chini
Bongo hiyo
Juu hewani umbali wa inchi 38,000 elfu kutoka usawa wa bahari yaani zaidi ya kilomita 11juu, napata fursa ya kung'amua picha hizi ............


Picha ya juu inaonesha mto fulani karibu na uwanja wa ndege wa mwanza
  

Nikiwa hewani nikapata fursa ya kuinasa hospitali hii ya bugando jijini mwanza
Baada ya muda wa saa 1 na dk 16, boing la fast jet likatua jijini mwanza, watu bila uchovu tukakanyaga ardhi ya mwanza na kuanza majukumu mapya.
Hapa nakutana na usafiri wa vyombo vya majini kuelekea Nansio Ukerewe 
Mwalo wa Kimataifa wa Kirumba Mwaloni jijini mwanza

Siku hii magugu maji yalikuwa ya kutosha Ziwani kama unavyoyaona mwenyewe
Baada ya safari ya masaa 3 na nusu chombo binafsi kinatia nanga katika bandari ya kujitegemea  Nansio mjini.
Hapa nikakuta gari za kubeba abiria aka michomoko zikiwa zimeumana na kusababisha ajali ambayo bahati nzuri haikusababisha vifo, japo majeruhi walikimbizwa hospitalini.

Baadhi ya maeneo mengine ya kisiwa hiki cha ukerewe usafiri wake ni wa kupanda mitumbwi kama huu pichani ambao niliushuhudia ukiwa umezidiwa na maji.
Baada ya majukumu yaliyonipeleka Ukerewe kukamilika nikarudi katika bandari binafsi ili kupanda feri hilo pichani ( la binafsi ) kurudi mwanza mjini.
heka heka za hapa na pale watu wakipakia mizigo na bidhaa za kibiashara kutoka kisiwani kwenda jijini mwanza,
Pembeni naiona bandari ya Nansio ikiwa na meli ya enzi za mwalimu, Mv clerias ikiwa inapakia abilia kwa upinzani na hii ya Mv Nyehunge ya binafsi wakati wa mchana tu.
Bandari ya Nansio hiyo
Sehemu ya feri nililopanda kwa safari zangu za nansio - ukerewe
Jiwe hili maarufu la Bismack Rock liko ufukweni mwa ziwa jijini mwanza barabara ya kuelekea  Capri Point
Hii ni sehemu ya bandari ya mwanza - North Port. Meli ya Mv Victoria ianonekana ikiwa imepaki kusubuiri abiria wanaosafiri kwenda bukoba kwa safari za usiku tu, kwani mchana siku hizi yapo mabasi mengi yanayopishana kwa safari za nenda rudi mwanza - bukoba.
Katika ziara yangu nafika eneo hili la buseresere chato

bomoa bomoa za ujenzi wa barabara ya bwanga to biharamulo
ofisi za vyama vyetu vya siasa huko chato
Nakutana na baadhi ya abiria wenzangu tukakwea fast jet bila karaha na kusafiri salama hadi dar
Sehemu ya nje ya ndege 5H - FJC  kabla ya safai yake kuja dar jioni  ikiwa ktk uwanja wa ndege mwanza