Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Mhe.Wilson Kabwe akiwatambulisha Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula kupitia CCM (katikati) na Naibu Meya Mhe.John Minja (CCM) muda mfupi baada ya kutangazwa washindi kufuatia uchaguzi uliofanyika leo katika ukumbi wa Halimashauri ya jiji la Mwanza.
Kikao cha Uchaguzi cha Halimashauri ya Manispaa ya Nyamagana jijini Mwanza kimemchagua Diwani wa Kata ya Mkolani Mhe. Stanslaus Mabula wa CCM kuwa Meya wa Jiji hilo baada ya kupata kura 11 na kumshinda mshindani wake wa chama cha CHADEMA Mhe. Charles Chinchibela aliyepata kura 8 tu.