Takriban watu arobaini na moja wameuawa na wengine arobaini kujeruhiwa katika shambulizi la bomu lililotokea nje ya msikiti katika eneo la Mkoa wa Maymana.
Shambulio hilo lilitekelezwa nje ya msikiti wakati waumini walipokuwa wakishereheka sikukuu ya Eidd el-Hajj. Maafisa wa serikali hawakujeruhiwa lakini polisi na wanajeshi ni miongoni mwa waliojeruhiwa.
Afisaa mmoja katika mkoa huo alisema kuwa gavana wa eneo hilo pamoja na mkuu wa polisi walikuwa ndani ya smikiti huo wakati wa shambulizi.
Walioshuhudia walisema kuwa mtu huyo wa kujitolea mhanga alikaribia msikiti na kutegua mabomu aliyokuwa amefungiwa kifuani baada ya sala ya Eid kukamilika, na waumini kusimama nje ya msikiti wakijuliana hali.
Haijulikani jinsi mtu huyo alivyoweza kupita vizuizi vinne kabla ya kufikia msikiti huo. Vizuizi hivyo vya usalama viliwekwa kwa sababu watu wanahofia kushambuliwa wakati huu wa sikukuu.
Afisa mmoja wa usalama alieleza kuwa mshambuliaji huyo alikuwa amevalia sare za polisi, ambazo huenda ziliwapumbaza maafisa wa usalama katika vizuizi hivyo.
Gavana wa Mkoa, wanasiasa wa vyeo vya juu na mkuu wa polisi walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakishiriki sala hiyo
Shambulio hilo limetokea siku chache tu baada ya kundi la wapiganaji kuwaua maafisa kadhaa wa Serikali katika Mkoa huo, kukiwemo aliyekuwa wakati mmoja afisa mkuu wa Taliban ambaye baadaye alijiunga na Serikali katika eneo la Faryab.
Shambulio hilo limetokea siku chache tu baada ya kundi la wapiganaji kuwaua maafisa kadhaa wa Serikali katika Mkoa huo, kukiwemo aliyekuwa wakati mmoja afisa mkuu wa Taliban ambaye baadaye alijiunga na Serikali katika eneo la Faryab.
Usalama umedumishwa kote nchini Afghanistan wakati huu wa siku kuu ya Eid.