October 29, 2012

Hillary Clinton ziarani Afrika




Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Hilary Clinton yuko nchini Nigeria, ili kuzungumzia swala la kukithiri kwa tisho la usalama kutokana na makundi ya wapiganaji wa kiisilamu katika nchi jirani ya Mali.
President Hillary Clinton
Mapema mwezi huu, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa,
ilipitisha azimio linalotoa mwanya wa kikosi cha pamoja cha muungano wa Afrika [AU],kuzima uasi Kaskazini mwa Mali.

Wapiganaji wa kiisilamu kutoka Algeria wanasemekana tayari wameingia nchini Mali kusaidia harakati za wapiganaji wa Tuaregambapo Algeria ni nchi muhimu katika eneo la Sahel kwa misingi ya kijeshi na kuungwa mkono kwake ni muhimu katika kuingilia kati mzozo wa Mali.
Aidha wapiganaji wa Mali,waliotumia mwanya wa usalama wakati wa mapinduzi yaliyofanyika mwezi Mei mjini Bamako kudhibiti eneo la kaskazini mwa Mali, imethibitika kuwa wana uhusiano wa karibu na kundi la al-Qaeda.
Balozi wa Marekani aliyesafiri na Bi.Clinton alisema kuwa swala la Mali limepewa kipaombele katika ajenda ya mazungumzo kati ya Bi Clinton na rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika pamoja na waziri wa mambo ya nje Mourad Medelci.
Algeria ilikuwa imeelezea wasiwasi kuhusu mipango ya shirika la ECOWAS, kutuma wanajeshi elfu tatu kupambana na wapiganaji Kaskazini mwa Mali kwa hofu ya kutikisa uthabiti wa eneo hilo.
Lakini Algeria ambayo ina jeshi kubwa zaidi katika eneo la Sahel, imekuwa ikionyesha dalili ya kutaka kuingilia kati mzozo huo.

Wiki jana kulikuwa na ripoti za makundi ya wapiganaji wa kigeni kutoka Ageria na Magharibi mwa jangwa la Sahara,kuanza kuwasili katika ngome za wapiganaji ya Timbuktu na Gao.
Chanzo:Bbc