October 29, 2012

UJUE UJI WA LAVA UNAOLIPUKA NA KUWAKA MOTO

Picha hii juu: Lava ikifukuta katika chanzo katika mlima wa mwamba. Mlima huu ni mawe ya sehemu ya lava iliyomwagika na kupoa kisha kuganda na kuwa ngumu kama mawe.

 Hapa lava ikimwagika katika muonekano huo mwekundu. Huo wekundu ni uji wa lava ya moto inayochoma ukitiririka kutafuta uelekeo mpya na baadae kupoa na kutengeneza miamba mipya ya mawe magumu.
Lava hii ni ile inayofukuta na kumwagika juu ya ardhi.Pia ipo Lava yenye tabia ya kufukuta na kumwagika chini ya kina kirefu cha Bahari ambapo humwagika na kupoa baharini na kutengeneza miamba mikubwa ya mawe.
Hata hivyo Mdau unashauliwa kufuatilia kwa karibu utafiti huu wa maajabu sana hapa duniani...
Fuatilia picha hapa chini.  
 Uji wa Lava ya moto ukimwagika Baharini na baadae kupoa kisha kuwa miamba migumu/mawe.