October 29, 2012

Kimbunga Sandy Chapiga Jijini New York Leo


Maafisa katika idara ya hewa nchini Marekani wamesema takribani watu milioni hamsini wataathiriwa na kimbunga hicho.

Kimbunga Sandy kilianza kupiga kutoka nchini 
Cuba wiki iliyopita ambako kilisababisha vifo vya watu takribani ishirini.







Jiji la New York limesemekana kuwa katika hatari  zaidi kuathirika kwa kimbunga hiki kwa sababu sehemu kubwa ya jiji hilo inazungukwa na bahari.
Sehemu nyingi za jiji zilifurika maji lakini watu waliendelea na shughuli zao ingawa kwa tahadhari sana.