October 21, 2012

MOTO WATEKETEZA DUKA DAR ES SALAAM LEO

Moto mkubwa umeliteketeza Duka maarufu la Vifaa vya Ujenzi katika Eneo la Tegeta Kwa Ndevu mnamo majira ya Alasiri na kusababisha hasara ya mamilioni ya shilingi. Shuhudia picha hizi ingawa ni masikitiko....
Umati wa mashuhuda wakitazama mali ikiendelea kuteketea katika duka hilo upande wa kushoto mwa picha hii.
kufa kufaana ..........
Mbinu butu pia zilionekana kutawala kuzima moto huo mkubwa
Ultimate Security walifika na kukuta sehemu kubwa ya duka hilo imeshika moto !
Hata hivyo mmiliki wa Duka hilo la Vifaa vya ujenzi maarufu hapo Tegeta Kwa Ndevu hakuweza kupatikana ili kutoa tathimini ya jumla ya mali yote iliyoteketea bure kwa  moto huo ambao chanzo chake hakiweza kufahamika mara moja.