Ni Afrika Kusini v/s Cape Verde fungua dimba Jan 19 mataifa Huru Afrika 2013
Wenyeji Afrika Kusini na Cape Verde zitachuana katika mechi ya ufunguzi wa fainali za kombe la mataifa Afrika hapo Januari 19, 2013 nchini Afrika Kusini. Ratiba ya makundi ilitangazwa nchini humo Jumatano usiku katika sherehe ambazo zilihudhuriwa pia na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Ratiba ya makundi inaonyesha kuwa wenyeji Afrika Kusini watakuwa katika kundi A pamoja na Cape Verde, Angola na Morocco. Kundi B litakuwa na nchi za Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Niger na Mali wakati mabingwa watetezi Zambia, Nigeria, Ethiopia na Burkina Faso watachuana katika kundi C. Kundi D litajumuisha timu za mataifa ya Ivory Coast, Togo, Algeria na Tunisia.Wachambuzi wa kandanda wanasema jinsi makundi hayo yalivyojitokeza katika fainali hizo hakuna kundi ambalo linaweza kusemwa kwa uhakika kuwa "kundi la kifo" kwani timu kubwa kama vile Ghana, Nigeria, Ivory Coast and wenyeji Afrika Kusini zote ziko katika makundi tofauti