Waathiriwa wa Ukimwi kuishi maisha marefu !
MTU ANAPOGUNDUA KWA MARA YA KWANZA KWAMBA AMEAMBUKIZWA VIRUSI VYA HIV HUPATWA NA MSHTUKO.
WENGINE HUONA KIFO KIMEPIGA HODI, WAKIHOFIA KUMWELEZA YEYOTE KUTOKANA NA UNYANYAPAA.! LAKINI LEO HII HALI IMEBADILIKA KWANI KUNA MATUMAINIMAPYA YA KUISHI BAADA YA UKIMWI. DOROTHY ONYANGO AMBAYE NI MUATHIRIKA WA HIV KUTOKA KENYA,NA MWENYEKITI WA SHIRIKA LA KINA MAMA WANAOISHI NA UKIMWI NCHINI KENYA LIITWALO WOFAK.Anaelezea kuwa maendeleo makubwa yamefikiwa kuwapa waathiriwa matumaini ya kuendelea kuishi na kwamba hivi leo kuna majaribio ya dawa mpya na chanjo. Hizi ni miongoni mwa habari njema kwa waathiriwa na wasio waathiriwa wa HIV AIDS. Anasema ana matumaini kuwa kizazi kisicho na ukimwi chawezekana,kinyume na ilivyokuwa miaka ya themanini na tisini, kwani sasa waathiriwa wa Ukimwi wamepata sauti.Wamepata dawa za kudhibiti gonjwa hilo na wanajua namna ya kujitunza na wanaishi maisha marefu kama watu wengine wowote.Ni kitu cha kawaida kwa muathiriwa kupatwa na mshtuko mara anapogundua ameambukizwa virusi vya HIV na Ukimwi na kuanza kujenga matumaini mapya ya kukabiliana na hali hiyo ya maambukizi. Dorothy ambaye ameishi na virusi hivyo kwa zaidi ya miaka 15 anaeleza kuwa aligunduliwa kuwa na virusi hivyo mapema miaka ya ‘90 wakati huko Kenya mabango makubwa ya watu waliokondeana kwa ukimwi yakiwekwa barabarani na vyombo vya habari kutahadharisha kuhusu ugonjwa huo. Hakumweleza mtu yeyote kuwa ana virusi vya HIV hadi baada ya miaka mitano.Ni vipi Dorothy alimudu kuishi miaka mitano baada ya kugundulika kuwa na HIV.
Je, alikula chakula cha aina gani au alikuwa na msukumo wa aina gani binafsi kuweza kuishi na kuficha ukweli juu ya hali yake bila kuonekana kuwa muathiriwa?Mama huyo anasema alikwenda kimya kimya kwenye mikutano ya waathirwa, na kusoma kila habari zilizoandikwa kuhusu ukiwmi. Alikula vyema na kujitunza. Na huko Kenya dawa ya Kemron iliyotangazwa kuwa inaweza kudhibiti maradhi hayo aliitumia. Alitumia pia dawa nyingine kwa jina Pearl Omega. Lakini baadaye akaamua kuzungumza na wakenya waliokuwa wamejitokeza wazi kueleza kuwa ni waathiriwa na hivyo kupata msaada wa kimawazo na madawa.Na kwa wale wanaogunduliwa na HIV na Ukimwi na kutangaza vita vya kusambaza virusi hivyo kwa wengine. Dorothy anawashauri wajilinde wenywe. Anatahadharisha kuwa wanaweza kudhoofisha afya yao zaidi kwa kupata maambukizo mengine ya zinaa na kukaribisha mauti kabla ya wakati wao.Anasema mtu akiwa muathirika hakuna njia ya kubadili hali yake kuwa si muathirika, na kwamba kilicho bora kufanya ni kutafuta msaada kuweza kuishi maisha marefu kwa kutumia madwa na kula vizuri. Dorothy ambaye amekuwa mwenyekiti wa chama cha wanawake wanaosihi na ukimwi nchini Kenya kinachojulikana kwa kifupi kama WOFAK, anawapa matumaini waathiriwa wa HIV na Ukimwi na anaandika kitabu kuhusu maisha yake na wanawake wengine walioathiriwa lakini wanaoishi maisha ya kawaida.Na kwa hakika ikiwa wewe ni muathiriwa au una mtu aliyeathirika na virusi vya HIV na Ukimwi fahamu kwamba yapo matumaini na mifano dunia hii na haswa Afrika ni chungu nzima. Ishi kwa matumaini
.