Obama na Romney wachuana vikali
Rais wa Marekani Barack Obama na mpinzani wake Mitt Romney wamepambana katika mdahalo wa tatu na wa mwisho huku Bw.Obama akisema mapendekezo yote ya sera ya mambo ya nje ya Romney yamekuwa ni makosa.
Gavana huyo wa zamani wa Massachusets alijibu mashambulizi kwa rais Jumatatu usiku katika jimbo la Florida akisema kumkosoa si ajenda kwa kuzuia ghasia katika mashariki ya kati.
Bw.Romney alikosoa sera za Obama za mambo ya nje akisema ameona kurudi nyuma kwa kiasi kikubwa kwa aina ya matumaini tuliyokuwa nayo.Bw.Obama amesema Marekani imefanya kazi kubwa na washirika wake kuleta amani na demokrasia katika eneo hilo na kuitaja Libya kama mfano.
Kuhusu Iran Obama amesema utawala wake umeonyesha uwezo kwa kuweka vikwazo vikali kuliko vyote katika nchi hiyo ya kiislam.