October 27, 2012

ON MY LOVELY BIRTHDAY


 YAKUBU K .M'KAKA,
Hapa ndipo Kiijongo, kijijini  nilipozaliwa na kuishi miaka kadhaa kabla ya kujongea katika Majiji Kadhaa hapa nchini na kwingineko.
Tarehe 26 Oktoba 2012, nimeadhimisha siku ya kuzaliwa kwangu na kutimiza miaka kadhaa ya maisha yangu hapa duniani.
Binafsi namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia katika kila hatua ya Maisha yangu. Ni Mungu wa pekee anayetujalia kwa kila jambo katika maisha yetu ya kila siku ya leo na ya baadae na milele Daima... 
Wadau msijiulize kwangu kuadhimisha siku kuu yangu ya kipekee katika maisha, kwa kimya kimya !!! kwani niliamua kuiadhimisha siku hii muhimu kwangu kwa kwenda Home Kijiji cha Kiijongo Kata ya Kaibanja Tarafa ya Katoro Wilaya ya Bukoba Vijijini ambako ilinichukua masaa kadhaa kwenda kupiga picha hizi muhimu kwangu nikiwa na Mzazi wangu pekee [Baba] na ndugu jamaa na marafiki hapo kijijini. Pia nilipata fursa ya kutembelea kaburi la Marehemu Mama yangu ambaye alikwisha tangulia mbele ya  Haki.
Dar-Mwanza nilikwenda kwa ndege ya kampuni ya Ndege 540 kwa Return Ticket na kuchukua usafiri binafsi hadi Home!
Yawezekana Mdau ukagusika na simulizi hii ya maisha yangu binafsi......japo hata mimi naamini kila mtu hapa Duniani anasimulizi ya maisha yake tena inayogusa huruma /furaha za watu wengine kwa upekee mkubwa....
TUKUMBUKE NYUMBANI HATA IKIWA NI KIJIJINI..............................!