Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ0 ambazo zilikutwa kwenye begi la watu watano ambao wanasadikiwa kuwa ni majambazi .Tukio hilo lililtokea katika eneo la Olmatejoo jijini Arusha leo asubuhi na Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi Watatu kati yao ambao baadae walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali .
MNAMO TAREHE 22/11/2012 MUDA WA SAA 3:45 ASUBUHI KATIKA ENEO LA OLMATEJOO HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA, WATU WATATU (AMBAO MAJINA YAO BADO HAYAJATAMBULIKA) WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WALIUAWA NA ASKARI WA JESHI LA POLISI WAKATI WA WAJIBIZANO YA KURUSHIANA RISASI.
TUKIO HILO LILITOKEA MARA BAADA YA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA KUPATA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA AMBAO WALIELEZA KWAMBA, KATIKA ENEO HILO KULIKUWA NA WATU WATANO AMBAO WANAWATILIA SHAKA, NDIPO BAADHI YA ASKARI WALIKWENDA KATIKA ENEO HILO KWA AJILI YA KUFANYA UCHUNGUZI.
MARA BAADA YA ASKARI HAO KUFIKA ENEO HILO, WATU HAO WALISHTUKA NA MMOJA WAO ALIYEKUWA NA SILAHA AINA YA BASTOLA KIUNONI ALIITOA NA KUANZA KUWAFYATULIA RISASI ASKARI HAO.
KUTOKANA NA HALI HIYO ASKARI HAO WALIAMUA KUJIBU MAPIGO NA KUFANIKIWA KUWAJERUHI WATU WATATU KATI YA WATANO NA WENGINE WAWILI WALIFANIKIWA KUKIMBIA PAMOJA NA BASTOLA.WATU HAO WALIFARIKI DUNIA WAKIWA NJIANI WANAPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA MOUNT MERU KWA AJILI YA MATIBABU. ASKARI HAO WALIFANIKIWA KUPATA BEGI LILILOTUPWA NA WATU HAO NA MARA BAADA YA KUPEKUA WALIKUTA BUNDUKI MBILI; MOJA AINA YA SHORTGUN NA NYINGINE AINA YA RIFLE YENYE NO. 08805 AMBAYO ILIKUWA IMEKATWA MTUTU PAMOJA NA KITAKO.
MBALI NA BUNDUKI HIZO PIA WALIKUTWA NA RISASI 16 ZA SHORTGUN, KITAKO NA MTUTU WA BUNDUKI AINA YA RIFLE, MTALIMBO (KIPANDE CHA CHUMA) AMBACHO KINASADIKIWA KUWA KINATUMIWA KATIKA SHUGHULI ZA UVUNJAJI, RUNGU MOJA, PANGA MOJA, TUPA TATU ZA KUNOLEA PANGA, SARE ZA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) AMBAZO NI SURUALI MOJA, T-SHIRT MOJA NA KOFIA MOJA.
PIA ZILIPATIKANA KOFIA MBILI ZINAZOTUMIKA KUFICHA USO PAMOJA NA KITAMBULISHO VYA KUPIGIA KURA, LESENI YA UDEREVA NA KITAMBULISHO CHA MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI DODOMA.MPAKA HIVI SASA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA LINAENDELEA KUWATAFUTA WATU WAWILI AMBAO WALIKIMBIA NA PIA LINAFANYA JITIHADA ZA KUWATAMBUA WATU WALIOUAWA AMBAPO MPAKA HIVI SASA MIILI YAO IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA MOUNT MERU.
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI,
(ACP) LIBERATUS SABAS
TAREHE 22/11/2012.