November 21, 2012

 MAADHIMISHO YA SIKU YA MAOMBI NA VITENDO KWA WATOTO DUNIANI
Maadhimisho ya Siku  ya Maombi na Vitendo kwa Watoto  Duniani  ambapo  watoto  kutoka katika shule mbalimbali Dar esSalaam wamekutana kuadhimisha  siku hiyo kwa sala na maombi wakiunganana wawakilishi  kutoka  katika madhehebu mbalimbali. Aidha, Kabla yamaadhimisho hayo  watoto kupitia vilabu vyao vya shule za sekondari namsingi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar  walipata nafasi ya kuwa nakongamano kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu watoto na  hivyokutoka  na  Maazimio ambayo wameyawasilisha leo kwa Serikali na wadaumbalimbali wanaoshughulika na masuala ya Watoto.

Naibu Waziri Ummy Mwalimu pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la UNICEF Tanzania . Bw. Jamal Gulaid katika picha ya pamoja na wawakilishi wa vilabu vya watoto wa shule za msingi kutoka shule mbalimbali na wageni waalikwa


Wanafunzi wa shule ya Buguruni Viziwi wakionesha mchezo kuhusu Ukatili kwa Watoto