November 27, 2012


Pamoja na Kupewa shinikizo la kuondoka,  M23 wasema''Katu hatuondoki Goma'' 

Askari Waasi wa M23 wamewalazimisha watu kutoroka makazi yao mjini Goma Mahariki mwa DRC
Viongozi wa waasi wa M23 ambao wiki jana waliuteka mji wa Goma Mashariki mwa DRC, wanasema katu hawataondoka Goma hadi serikali itakapotimiza matakwa yao.
Kiongozi wa kundi hilo, Jean Marie Runiga alisema kuwa wapiganaji wake wataondoka mara moja ikiwa Rais Joseph Kabila, ataitikia matakwa yao ambayo ni pamoja na kuivunja tume ya uchaguzi.
Serikali ya Congo hata hivyo imepuuza matakwa hayo kuwa hayana tija kwa Taifa kwa sasa .
Uganda ambayo imekuwa ikipatanisha pande hizo mbili kwenye mkutano mjini Kampala, awali ilisema Waasi hao tayari walikubali kuondoka Goma bila vikwazo.
Siku ya Jumamosi, serikali za nchi za Maziwa Makuu ziliwapatia waasi hao Masharti ya siku mbili kuondoka mjini Goma.