December 17, 2012


ALIEPATA AJALI NA KUDHANIWA KUWA AMEKUFA, AFUNGA NDOA JIJINI MBEYA JANA

Mungu ni Mkubwa
Bwana harusi Emmanuel Mwangosi akiwa na mkewe Magreth  Mtebe mara tu baada ya kufunga pingu za maisha jana katika kanisa la Agape jakaranda jijini mbeya.Bwana harusi huyu alipata ajali usiku wa kuamkia jumamosi,eneo la Mafiati jijini Mbeya,wakati akiwa na pikipiki yake akielekea kanisani kulikokuwa na mkesha wa ibada na sherehe za harusi hiyo.

Hapa bwana harusi akimvisha mkewe pete ya ndoa huku bibi harusi akiwa katika furaha kubwa na kumshukuru mungu kwa kumuepusha mumewe katika ajali mbaya iliyotokea siku moja kabla ya ndoa kufungwa
Hapa Maharusi wakipata maombi ya ndoa njema kutoka kwa wachungaji mbalimbali wa kanisa hilo la AGAPE
"Alichokiunganisha Mungu, binadamu asikitenganishe."
"Sasa tu mwili mmoja kitakachotutenganisha ni kifo tu, jina la bwana libarikiwe"
Bwana harusi akipokea cheti cha ndoa toka kwa mchungaji Mwasota

Maharusi wakiwa katika pozi la 'snap' na nyuso za furaha mara baada ya kufunga  pingu za maisha
Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na familia na wazazi wao.

IKUMBUKWE KUWA
Bwana Harusi alipata ajali mbaya sana na ikadhaniwa kuwa angepoteza maisha!
Lakini uweza wa Mungu ni mkubwa ....
Bwana Harusi alinusulika
Shuhudia picha za ajali yake ya pikipiki.
.