December 17, 2012


WANAWAKE WAJASIRIAMALI WA KATA YA KIPAWA WAPATA MAFUNZO YA UFUNDI STADI NA UJASIRIAMALI

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Dk. Makongoro Mahanga (aliesimama) akizungumza wakati alipokuwa akifungua Mafunzo ya Ufundi Stadi na Ujasiriamali kwa Wanawake wa Kata ya Kipawa yaliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Air Wing,Ukonga jijini Dar.Kulia ni Diwani wa Kata hiyo ya Kipawa na Mratibu wa Mafunzo hayo,Bonnah Kaluwa na kushoto ni Msaidizi wa Naibu Waziri,Bw. Mohamed na wa pili kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo,Said Fundi.
Diwani wa Kata ya Kipawa,Bonnah Kaluwa akimkaribisha Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Dk. Makongoro Mahanga kufungua mafunzo ya Wanawake Wajasiriamali wa Kata ya Kipawa.
Mgeni rasmi Dk. Makongoro Mahanga (wa tatu kushoto), Msaidizi wa Waziri,Bw. Mohamed, Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo Said Fundi (wa pili kushoto), Diwani wa Kata ya Kipawa, Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Lucy Semendu (kulia) na Mwakilishi kutoka Kampuni ya Darling ambao ni wadhamini wa mafunzo hayo wakipiga makofi kabla ya kufunguliwa rasmi kwa mafunzo hayo.
Wakina mama wajasiriamali wa Kata ya Kipawa Manispaa ya Ilala wakishangilia wakati semina yao ya siku moja ya mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika ukumbi wa Air Wing Dar es Salaam ikiendelea. Semina hiyo ilifadhiliwa na Benki ya Equity na Darling Hair kwa msaada wa Diwani wa Kata hiyo Bonnah Kaluwa.
wanawake hao Wajasiriamali wakijiandikisha kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo.
Wakina mama hao wakiwa katika mafunzo hayo

IKULU YAZAWADIA WAFANYAKAZI WAKE BORA, YAPOKEA MAKOMBE YA SHIMIWI NA KUPONGEZA WANAMICHEZO WAKE LEO

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipozi na kikosi kizima cha michezo mbalimbali cha Ikulu Sports Club ambacho kilinyakua jumla ya makombe matano katika michezo mbalimbali ya Shirikisho la Michezo ya Wizara (SHIMIWI) mwaka huu mjini Morogoro. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma za Ikulu Bw Julius Mogore katika hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora iliyofanyika leo Deswemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam. Kwenye michezo hiyo iliyofanyika kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba 10 mwakq huu, ilishirikisha jumla ya wanamichezo 3500 kutoka wizara 56, mikoa 18 na idara za serikali 14 ambapo wanamichezo 91 wa Ikulu walioshiriki walifanikiwa kuibuka washindi wa kwanza katika michezo ya Baiskeli, Netbal, Kuvuta kamba wanawake na wanaume na kushik nafasi ya pili ya riadha kwa wanawake na wanaume.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akinyanyua juu mojawapo ya makombe matano ambayo Ikulu Sports Club ilinyakua kwenye michezo ya SHIMIWI ya maka huu mjini Dodoma katika hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam. Kwenye michezo hiyo iliyofanyika kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba 10 mwakq huu, ilishirikisha jumla ya wanamichezo 3500 kutoka wizara 56, mikoa 18 na idara za serikali 14 ambapo wanamichezo 91 wa Ikulu walioshiriki walifanikiwa kuibuka washindi wa kwanza katika michezo ya Baiskeli, Netbal, Kuvuta kamba wanawake na wanaume na kushik nafasi ya pili ya riadha kwa wanawake na wanaume.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwa katika picha na Bw. Miraji Ahmed Saleh ambaye ameibuka kuwa mfanyakazi Bora na Hodari kwa mpigo, akiwa kama Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi katika Idara ya Huduma za Ikulu na Zahanati katika hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi akiwa na Mwadawa Twalibu, Sophie Komba na Pascalia Kibayasa ambao wachezaji wa timu ya netball ya Ikulu Sports Club ambao pia ni wachezaji wa timu ya taifa ya mchezo huo (Taifa Queens) kwenye hafla ya kuwazawadia iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwa katika picha na Bw. Miraji Ahmed Saleh ambaye ameibuka kuwa mfanyakazi Bora na Hodari kwa mpigo, akiwa kama Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi katika Idara ya Huduma za Ikulu na Zahanati katika hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwa na Mwadawa Twalibu, Sophie Komba na Pascalia Kibayasa wachezaji wa netball wa Ikulu Sports Club ambao pia ni wachezaji wa timu ya Taifa (Taifa Queens) ya mchezo huo kwenye hafla ya kuwazawadia iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa nane toka kulia ) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi (kulia kwake) na Mkurugenzi wa Huduma za Ikulu Bw Julius Mogore (wa pili kushoto ) pamoja na mwenyekiti wa TUGHE tawi la Ikulu Bw. Paulo Mgeni (kulia) wakiwa na Mwadawa Twalibu, Sophie Komba na Pascalia Kibayasa ambao wachezaji wa timu ya netball ya Ikulu Sports Club ambao pia ni wachezaji wa timu ya taifa ya mchezo huo (Taifa Queens) kwenye hafla ya kuwazawadia iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU.