December 09, 2012


Rais Zuma amtembelea Mzee Mandela hospitalini

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amemtembelea rais wa zamani wa nchi hiyo ,Mzee Nelson Mandela, hospitali mjini Pretoria.

Nelson Mandela
Hapo awali wakuu wa serikali walisema Mzee  Mandela mwenye miaka 94 alilazwa hospitalini Jumamosi kwa uchunguzi wa kiafya, na kwamba hali yake siyo ya kutia wasiwasi.Rais Zuma alisema Mzee Mandela alimkuta katika hali nzuri baada ya kupumzika usiku kucha.
Mara ya mwisho Mzee Mandela alilazwa hospitalini mwezi Februari mwaka huu akitibiwa kwa matatizo ya tumbo aliyokuwa nayo kwa muda mrefu.
Hata hivyo Mzee Mandela haonekani hadharani mara kwa mara tangu Afrika Kusini ilipofungua michezo ya Kombe la Dunia mwaka wa 2010.